1. Utangulizi

Kituo cha Rasilimali na Usaidizi (RSH) cha Kulinda Usalama kinaendeshwa na muungano wa mashirika, ikijumuisha Options, SDD, GCPS, Terre des hommes na Sightsavers.

Unapotembelea RSH, habari inayohusiana na kurasa utakazoangalia huenda ikahifadhiwa kwenye vidakuzi vilivyowekwa kwenye kifaa kinachotumika kufikilia RSH au kutumia teknolojia sawa kama vile pikseli za kufuatilia. Sera hii ya vidakuzi inaeleza vidakuzi na pikseli za kufuatilia ni nini, vidakuzi na pikseli za kufuatilia tunazotumia, tunazitumia kufanya nini, na jinsi unaweza kubadilisha mpangilio wako kuhusiana na vidakuzi na pikseli za kufuatilia tunazotumia.

Habari hii kuhusu vidakuzi inapaswa kusomwa kwa pamoja na Sera yetu ya Faragha ambayo inaeleza jinsi na kwa nini tunakusanya, kuweka, kutumia na kusambaza habari yako ya kibinafsi kwa ujumla, pamoja na haki zako kuhusiana na habari yako ya kibinafsi na habari zaidi kuhusu jinsi unaweza kuwasiliana nasi na mamlaka husika za usimamizi ikiwa una malalamishi.

Tunaweza kubadilisha sera hii ya vidakuzi mara kwa mara na kuchapisha matoleo yaliyosasishwa kwa RSH husika pamoja na taarifa za mabadiliko pale panapofaa.

2. Je, kidakuzi ni nini?

Vidakuzi ni faili za maandishi ambazo - kulingana na mipangilio yako - zinaweza kuhifadhiwa kwenye diski kuu ya kifaa chako (iwe kompyuta, tableti, simu ya mkononi au kifaa chochote kinachoweza kufikia mtandao) unapotembelea tovuti au kubonyeza tangazo. Vidakuzi hutumika kutambua kifaa ambacho vimehifadhiwa na hufanya kazi kwa muda mfupi tu.

3. Kwa nini tunatumia vidakuzi?

Kuna aina tatu tofauti ya vidakuzi ambayo inaweza kuhifadhiwa kwenye kifaa chako wakati unavinjari RSH. Matumizi ya kila aina imeelezwa hapa chini.

i. Vidakuzi muhimu

Vidakuzi muhimu husaidia RSH kufanya kazi kwa kuwezesha utendakazi wa kimsingi unaohitajika ili kutumia tovuti, kufikia maeneo salama, kuthibitisha watumizi na matumizi ya fomu za mawasiliano pamoja na utendakazi mwingine ulioboreshwa. Aina hii ya kidakuzi haiwezi ikazimwa. Unaweza kupanga kivinjari chako kuzuia au kukujulisha kuhusu vidakuzi hivi ila ikiwa utazuia matumizi yao, baadhi ya sehemu za RSH hazitafanya kazi.

ii. Vidakuzi vya kipindi

Vidakuzi vya kipindi hukubalisha RSH kuunganisha vitendo vyako wakati wa kipindi fulani katika kivinjari. Vidakuzi hivi vitakamilisha muda wao kila unapofunga kivinjari chako na havitasalia kwenye kifaa chako hapo baadaye.

iii. Vidakuzi vya utendakazi

Vidakuzi vya utendakazi huturuhusu kuhesabu ziara na vyanzo vya ziara hizo ndivyo tuweze kupima na kuboresha utendakazi wa RSH. Vidakuzi hivi hutusaidia kujua ni kurasa gani zenye umaarufu zaidi na zisizo na umaarufu na kutuonyesha jinsi wageni wanavyozuru tovuti yetu. Habari yote ambayo inakusanywa na vidakuzi hivi imejumlishwa na hivyo haionyeshi majina ya watumizi na hutumika tu kuboresha jinsi RSH itafanya kazi. Ikiwa hutaruhusu vidakuzi hivi, hatutafahamu ukizuru RSH na hatutaweza kufuatilia utendakazi wao.

iv. Ni vidakuzi gani tunavyotumia?

Jedwali lifuatalo linatoa habari zaidi kuhusu vidakuzi na pikseli za kufuatilia tunazotumia na ni kwa nini:

Aina Vidakuzi Muhimu

Kidakuzi cha kipindi cha Drupal - inaweka nambari ya Utambulisho wa kipindi ambayo inatambulisha mtumizi ambaye ameingia kwa wakati ule. Muda wake huisha baada ya kuondoka kwenye tovuti

 

Utendakazi

Google Analytics

Tunatumia hizi kurekodi na kuripoti matumizi ya tovuti. Sisi huficha IP ya wageni wote hadi kwa kiwango cha nchi asili kutumia nambari inayopachickwa lebo ya google ili tusirekodi data yoyote yako inayoweza kukutambulisha kibinafsi. Tunahakikisha kuwa tunapunguza kile kinachorekodiwa na kuzima kufuatiliwa na Google adwords.

Podbean

Tunaweka vidakuzi vya kimsingi visivyoonyesha jina ya mtumizi ili kutusaidia kuhesabu ni mara ngapi podikasti zetu zinasikilizwa kutumia huduma ya Podbean.

 

 

 

Hii ni nambari inayozalishwa kiotomatiki kama SESSffbcdb67dca02d807e3b6c5a8861ed54   

_gat _ga _gid __atuvc
__atuvs
AWSELBCORS
AWSELB
PBSECURESUSID

v. Idhini ya kutumia vidakuzi

Tunaomba ruhusa yako (idhini) ili kuweka vidakuzi, pikseli za kufuatilia na teknolojia yoyote iliyo sawa kwenye kifaa chako isipokuwa pale ambapo vitu hivi vina umuhimu kwetu ili tuweze kukupa huduma uliyoomba (kama vile kukusaidia kuweka bidhaa zako kwenye kikapu cha kununulia bidhaa na kutumia utaratibu wa kulipia bidhaa zile).

Kuna taarifa kwenye tovuti ya RSH inayoeleza jinsi tunatumia vidakuzi na kukuomba idhini ili kuweka vidakuzi kwenye kifaa chako.

4. Ninawezaje kudhibiti vidakuzi na pikseli za kufuatilia?

Kubadilisha mipangilio yako kupitia Kituo chetu cha Mapendeleo ya Vidakuzi

Kituo cha Mapendeleo ya Vidakuzi kinaweza kutumika kubadilisha mapendeleo yako ya vidakuzi kwa wakati wowote kulingana na mahitaji na upendeleo wako. Kifaa hiki hurekodi idhini yako na hasa kudhibiti utendakazi na kulenga vidakuzi vilivyoamilishwa wakati wa kutumia RSH.

Ikiwa ungependa kuweka vikwazo au kuzuia matumizi ya vidakuzi kwa jumla, unaweza kusanidi kivinjari chako ili kikupatie ujumbe wa ilani kila mara wakati kidakuzi kinataka kuhifadhiwa au unaweza kuzuia vidakuzi vyote. Pia, unaweza kufuta vidakuzi vyote ambavyo tayari vimetumwa kupitia kivinjari chako. Kwa habari ya jinsi unaweza kufanya hivi, tafadhali rejelea sehemu za 2 na 3 zilizoko hapa chini.

Ili kusaidia kurambaza kwa urahisi, RSH inapendekeza kuwa ukubalishe vidakuzi kwenye tovuti na usivifute. La sivyo, baadhi ya vipengele vya RSH huenda visionyeshe au kufanya kazi vizuri.

Kubadilisha mipangilio yako kwenye vivinjari tofauti

Udhibiti wa vidakuzi hutofautiana kutoka kivinjari kimoja hadi kingine. Tumia menyu ya msaada ya kivinjari chako ili kufahamu jinsi ya kubadilisha mipangilio ya vidakuzi vyako, au ubonyeze kiunganishi husika hapa chini:

Vidakuzi vya kutoka kwingine na jinsi ya kuvizuia

Kuzuia vidakuzi vinavyopima hadhira

Vidakuzi vinavyopima hadhira vimewekwa kwenye tovuti yetu na Google Analytics. Unaweza kuzuia vidakuzi hivi maalum kwa kubonyeza kwenye kiunganishi cha kuzima kilicho hapa chini, kupakua programu-jalizi na kuiweka kwenye kivinjari chako. Programu hii jalizi inaweza kutangamana na vivinjari vifuatavyo: Internet Explorer, Chrome, Firefox, Safari na Opera.

Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kuzima Google Analytics na kuweka programu-jalizi kwenye kivinjari, bonyeza hapa: Programu-jalizi ya kutoa Google Analytics kwenye kivinjari

Tafadhali kumbuka kuwa programu hii jalizi itahifadhi kidakuzi kwenye kifaa chako, ila kidakuzi hicho kitatumika tu kuzuia kivinjari chako kusafirisha data kwenda kwa Google Analytics.

Kwa habari zaidi kuhusu jinsi ya kuzima Google Analytics na kuweka programu-jalizi kwenye kivinjari, bonyeza hapa: Programu-jalizi ya kutoa Google Analytics kwenye kivinjari

Kwa habari zaidi kuhusu habari za faragha ya Google Analytics, bonyeza hapa: Kulinda usalama wa data yako

Kuzuia vidakuzi vya mitandao ya kijamii

Ili kuzuia vidakuzi vinavyotumiwa na mitandao ya kijamii (kama vile kupitia vitufe vya kushiriki), fuata maagizo yaliyoko kwenye viunganishi hapa chini:

Kuzuia vidakuzi hakutazuia moja kwa moja pikseli za kufuatilia kutuma habari kwenye seva ya pikseli. Unaweza kuzuia mpangilio huu kwenye kivinjari chako kuwa kizuizi iwezekanavyo yenye kuongezewa picha kutoka nje kwa kubadilisha mipangilio yako ya mfumo wa ulinzi na/au kutumia viendelezi fulani vya kivinjari. Hata hivyo, hii inaweza kuzuia utendakazi mwingine.

5. Jinsi ya kuwasiliana nasi

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusiana na habari hii ya vidakuzi au habari tuliyo nayo kukuhusu. Ikiwa ungependa kuwasiliana nasi, tafadhali tuma baruapepe kwa info@tdh-europe.org