Ili kupata kozi za Mafunzo kwa njia ya Mtandaoni za RSH, unahitaji kuwa umesajili akaunti ya mtumiaji nasi na kuingia.

 

Learning

 

RSH inaandaa msururu wa moduli tano za mafunzo kwa njia ya mtandaoni unaoitwa Masuala ya Kulinda Usalama. Moduli hizi zinatumia mafunzo kwa msingi wa vielelezo kueleza hadithi ya shirika la asasi ya kiraia la kufikirika linaloitwa Family Health Frontiers (FHF). Katika moduli hizi tano, wanafunzi wanajiunga na timu ya FHF wanapolenga kuwa shirika salama na kukabiliana na changamoto za kulinda usalama.

Kila moduli itaambatana na arifa za kulinda usalama ambazo zitatoa nyongeza za vichocheo vya mafunzo kwa hadi miezi miwili baada ya moduli kukamilika.

Moduli hizi zinalenga wataalamu wasio wa kulinda usalama katika Asasi za Kiraia (CSOs) ambao wanataka njia rahisi ya mafunzo, kujifunza ukweli muhimu kuhusu kulinda usalama, kupata maarifa, kutekeleza shughuli na kupata cheti cha RSH. Wataalamu wa kulinda usalama pia watafaidika kutoka kwa habari ya kiufundi, viungo kwa rasilimali za kusaidia na uwezo wa kujifahamisha kwa changamoto za kulinda usalama zinazokabili Asasi za Kiraia. Wale wote wanaofanya kazi katika sekta za maendeleo na kibinadamu watapata kuwa moduli hizi ni muhimu. 

Onyo

Moduli hizi zina yaliyomo ambayo unaweza kuyaona yanahuzunisha.

Moduli mbili za kwanza zinapatikana sasa kwa Kiingereza na Kifaransa. Moduli zilizobaki na arifa za kulinda usalama za RSH zitapatikana kwa Kiamhari, Kiswahili, Kiarabu na Kihausa mwaka wote wa 2021.

Unaweza pia kukamilisha kozi nje ya mtandao. Ili kupakua moduli katika muundo wa PDF, bonyeza hapa [https://safeguardingsupporthub.org/sw/documents/rsh-e-learning-offline-safeguarding-matters].

Utangulizi kwa Moduli ya 1

Masuala ya Kulinda Usalama Moduli ya 1: Kuanza

Hii ni moduli ya kwanza ya msururu wa sehemu tano za mafunzo kwa njia mtandaoni kuhusu kulinda usalama. Msururu unatanguliza dhana muhimu za kulinda usalama kupitia hadithi ya FHF - shirika la kitaifa la asasi ya kiraia linaloshughulikia masuala halisi ya kulinda usalama.

Jukumu lako ni kushirikiana na washiriki wa timu ya FHF inapofanya kazi kuhakikisha ulinzi dhidi ya Unyonyaji wa Kijinsia, Dhuluma na Unyanyasaji wa Kijinsia umejumuishwa kama sehemu muhimu ya programu mpya.

Malengo ya Mafunzo

Moduli hii itakusaidia:

  • Kufafanua masharti ya kulinda usalama;
  • Kuelewa majukumu ya kulinda usalama ndani ya shirika;
  • Kutambua umuhimu wa tabia za mahali pa kazi katika kulinda usalama.

Muda wa mafunzo: Dakika 30.

 

Utangulizi kwa Moduli ya 2

Masuala ya Kulinda Usalama Moduli ya 2: Kuanzia na washirika

Katika Moduli ya 2, wanafunzi wanaendelea kuandamana na FHF, wanapowasilisha pendekezo la ufadhili wa programu mpya, kukamilisha tathmini ya matakwa na kutambua washirika wa programu. Kulinda usalama katika hatua zote za usimamizi wa programu na hatari za kulinda usalama zimezungumziwa.

Malengo ya Mafunzo

Moduli hii itakusaidia:

  • Kuelewa umuhimu wa matakwa ya kulinda usalama kwa mashirika na washirika;
  • Kutambua shughuli muhimu za kulinda usalama ndani ya hatua zote za programu kwa kutekeleza programu kwa salama; na 
  • Kutambua hitaji la uongozi thabiti na desturi ya shirika kuelekea kwenye matendo yaliyo salama.

Muda wa mafunzo: Saa 1.

Unapokamilisha moduli hizi, unaweza kushiriki mawazo, maswali na maoni yako kuhusu ulichojifunza na wenzako kwenye Jukwaa la majadiliano ya Jamii kwa njia ya mtandaoni.